IAEA: Kuna uwezekano magaidi watatumia silaha za nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i3826-iaea_kuna_uwezekano_magaidi_watatumia_silaha_za_nyuklia
Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) umetadharisha juu ya uwezekano wa makundi ya kigaidi kutumia silaha hatari za nyuklia katika harakati zao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 26, 2016 03:47 UTC
  • IAEA: Kuna uwezekano magaidi watatumia silaha za nyuklia

Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) umetadharisha juu ya uwezekano wa makundi ya kigaidi kutumia silaha hatari za nyuklia katika harakati zao.

Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo amesema: “Ugaidi unasambaa kwa kasi kubwa mno na uwezekano wa kutumika silaha za nyuklia hauko mbali.”

Amano ameziasa nchi wanachama wa IAEA kushirikiana kuhakikisha kuwa dunia inakua pahala salama kutokana na silaha za maangamifu za nyuklia.

Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki umerekodi kesi 2,800 za magendo ya mada za silaha za nyuklia katika sehemu mbalimbali duniani tangu kati kati ya miaka ya 90.

Utawala haramu wa Israel ambao unamiliki vichwa vya nyuklia kati ya 200-400, umekataa katakata kuruhusu uchunguzi ufanyike dhidi ya vituo vyake vya kijeshi mbali na kukataa kusaini makubaliano ya kuzuia utengenezaji na usambazaji silaha za nyuklia NPT.

Marekani ndiyo nchi pekee duniani ambayo imewahi kutumia mabomu ya nyuklia dhidi ya miji ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1945.