Ripoti: Trump amesema uwongo mara elfu 2 ndani ya siku 347
https://parstoday.ir/sw/news/world-i38431-ripoti_trump_amesema_uwongo_mara_elfu_2_ndani_ya_siku_347
Ripoti mpya iliyochapishwa na gazeti la The Washington Post imesema Rais Donald Trump wa Marekani amesema urongo karibu mara elfu mbili ndani ya siku 347 alizohudumu ndani ya Ikulu ya White House.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 02, 2018 11:25 UTC
  • Ripoti: Trump amesema uwongo mara elfu 2 ndani ya siku 347

Ripoti mpya iliyochapishwa na gazeti la The Washington Post imesema Rais Donald Trump wa Marekani amesema urongo karibu mara elfu mbili ndani ya siku 347 alizohudumu ndani ya Ikulu ya White House.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumatatu, Trump ambaye ana mazoea ya kujikariri ametoa madai yasiyo na msingi takriban mara 60, na kuyakariri kwa zaidi ya mara tatu.

Ripoti hiyo imesema mwanasiasa huyo wa Republican amesema urongo mara 61 kuhusu masuala ya ajira na uwekezaji, huku akidanganya mara 33 kuwa Marekani ni moja ya nchi zinazotoza ushuru na kodi ya juu duniani.

Trump akinong'onezewa jambo na makamu wake, Mike Pence

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya gazeti la The Washington Post, Trump 'ameshangilia na kupongeza' kuimarika kwa soko la hisa, licha ya kusisitiza wakati wa kampeni kuwa soko hilo litaporomoka wakati Benki Kuu ya Marekani (Federal Reserve) itaanza kuongeza ada za riba.

Trump amekuwa akikosolewa vikali kwa kutoa madai ya uwongo na ya kukinzana.

Miezi michache iliyopita, James Comey, Mkuu wa zamani wa Polisi ya Federali ya Marekani (FBI) alisema Trump ni mrongo na kidhabi.