De Niro: Trump ni mpumbavu na mwendawazimu
Mkurugenzi na mtayarishaji maarufu wa filamu wa Marekani amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni mpumbavu na mwendawazimu.
Robert De Niro amekosoa mashambulizi ya mara kwa mara ya Donald Trump dhidi ya vyombo vya habari na kusema: Trump ni mtoto anayeongoza nchi na anataka kuvizingira vyombo vya habari kupitia njia ya kuvizidishia mashinikizo.
De Niro ameashiria kashfa ya Watergate iliyopelekea kusailiwa rais wa wakati huo wa Marekani, Richard Nixon na kulazimika kujiuzulu na kusema: Hivi sasa pia jamii ya Marekani na vyombo vya habari vinafanya jitihada za kujitenga na Donald Trump.
Mkurugenzi na mtayarishaji filamu huyo wa Marekani amekuwa akimkosoa sana Donald Trump na kumtaja kuwa ni mbaguzi. Alisema anatamani kumpiga ngumi usoni.
Matamshi na hatua zinazochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani zinaendelea kukosolewa sana na wasoni, wanasiasa na watu mashuhuri ndani na nje ya Marekani.
Kwa sasa kuna mjadala mkubwa nchini humo kuhusu usalama na uzima wa kiakili na kinafsi wa Trump na kunatolewa miito ya kuchunguzwa uwezo wake wa kiakili.