Mmishonari wa Marekani afungwa miaka 40 kwa kunajisi mayatima
https://parstoday.ir/sw/news/world-i38807-mmishonari_wa_marekani_afungwa_miaka_40_kwa_kunajisi_mayatima
Raia wa Marekani kutoka jimbo la Arkansas ambaye alikuwa anafanya kazi kama mmishonari nchini Haiti amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi mabinti wakiwemo wa umri wa miaka sita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 11, 2018 04:17 UTC
  • Mmishonari wa Marekani afungwa miaka 40 kwa kunajisi mayatima

Raia wa Marekani kutoka jimbo la Arkansas ambaye alikuwa anafanya kazi kama mmishonari nchini Haiti amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi mabinti wakiwemo wa umri wa miaka sita.

Taarifa ya Idara ya Sheria ya Marekani imesema kuwa, hukumu dhidi ya Daniel Pye mwenye umri wa miaka 36 ilitolewa jana Jumatano.

Mmishonari huyo alipatikana na hatia mwezi Novemba mwaka jana, ambapo alikuwa anakabiliwa na mashitaka matatu, likiwemo la kusafiri katika nchi ya kigeni kwa lengo la kushiriki ngono na watoto wadogo.

Mmishonari huyo anadaiwa kuwabaka mabinti wa hadi miaka 6

Pye anaripotiwa kuwanajisi mabinti waliokuwa katika kituo cha mayatima alichokuwa akisisimamia katika mji wa Jacmel nchini Haiti, kati ya mwaka 2006 na 2012. 

Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Marekani, takriban makasisi 6,900 wa Kanisa la Katoliki la Roma wanadaiwa kuwalawiti watoto wadogo 16,900 kati ya mwaka 1950 na 2011.