Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) zimeongezeka Marekani tangu Trump aingie madarakani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i40733-chuki_dhidi_ya_uislamu_(islamophobia)_zimeongezeka_marekani_tangu_trump_aingie_madarakani
Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kuwa tokea Donald Trump alipoingia madarakani, idadi ya makundi yenye chuki na Uislamu na ukubwa wa harakati zao vimeongezeka nchini humo.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Feb 22, 2018 13:17 UTC
  • Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) zimeongezeka Marekani tangu Trump aingie madarakani

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kuwa tokea Donald Trump alipoingia madarakani, idadi ya makundi yenye chuki na Uislamu na ukubwa wa harakati zao vimeongezeka nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya mtandao wa habari ya Middle East Eye, Kituo cha Sheria cha Hali ya Umasikini wa Kusini nchini Marekani (Southern Poverty Law Center) kimetangaza kuwa idadi ya makundi yanayoupiga vita Uislamu nchini Marekani imeongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wa urais wa Trump na kwamba kwa mwaka wa tatu mtawalia, idadi ya makundi hayo imeongezeka kutoka makundi 101 na kufika 114.

Kwa mujibu wa kituo hicho cha masuala ya sheria, makundi hayo yamezidi kupata nguvu tangu Trump alipotoa Amri ya Uhamiaji na kuonyesha kuyaunga mkono makundi ya wazungu wanaojikweza.

Ripoti ya kituo hicho inaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2014 na kuendelea, idadi ya makundi yenye misimamo ya chuki nchini Marekani imeongezeka kwa asilimia 20.

Kongamano la Waislamu wa Marekani la kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia)

Punde baada ya Donald Trump kuingia madarakani, serikali kuu ya Washington ilielekeza bajeti yake katika kuyapa nguvu makundi ya wazungu wanaojikweza ambapo mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita wa 2017 Rais huyo wa Marekani aliwatetea wazungu wanazi makatili waliojumuika katika mji wa Charlottesville na kutamka kinywa kipana kwamba: "miongoni mwao kunawatu wazuri sana".../