China yazionya nchi zinazofuata sera za kibiashara za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i41095-china_yazionya_nchi_zinazofuata_sera_za_kibiashara_za_marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa, ufuataji sera za kibiashara za Marekani unaofanywa na baadhi ya nchi katika uga wa kibiashara, utasababisha madhara kwa biashara ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 03, 2018 01:11 UTC
  • China yazionya nchi zinazofuata sera za kibiashara za Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa, ufuataji sera za kibiashara za Marekani unaofanywa na baadhi ya nchi katika uga wa kibiashara, utasababisha madhara kwa biashara ya kimataifa.

Hua Chunying ameyasema hayo ikiwa ni radiamali na jibu la serikali ya China kwa hatua ya Marekani ya kuzipandishia ushuru wa asilimia 500 bidhaa za vyuma na alumini zinazoingizwa nchini humo kutoka China ambapo amesema kuwa, kufuata sera hizo za kibiashara za Washington hakutakuwa na tija nyengine ghairi ya kuiletea madhara biashara ya kimataifa.

Mgogoro kati ya China na Marekani

Kuhusiana na suala hilo, awali Wizara ya Biashara ya China ilikuwa imetangaza kwamba ikiwa Marekani itataka kupandisha kodi kwa bidhaa zinazozalishwa na nchi hiyo, basi Beijing nayo itachukua hatua mkabala dhidi ya Marekani. Mzozo wa kibiashara kati ya Marekani na China ulishika kasi zaidi tangu alipoingia madarakani Rais Donald Trump wa Marekani, hasa kutokana na siasa za Washington za kuyaondoa mashirika ya China katika soko la biashara la Marekani kwa kupandisha maradufu ushuru kwa biadhaa za China zinazoingizwa nchini humo.

Viongozi wa China na Marekani

Kufuatia hali hiyo serikali ya Beijing iliwasilisha malalamiko yake kwa Shirika la Biashara Duniani WTO, dhidi ya hatua hiyo ambayo inakinzana na ushindani halali wa kibiashara. Kadhalika mwezi Januari mwaka huu serikali ya China iliuonya Umoja wa Ulaya kutokana na siasa mbaya za umoja huo dhidi ya Beijing na kusisitiza kwamba mienendo hiyo inaweza kuvuruga mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hiyo na umoja huo.