Wamarekani wakiri, walitungua ndege ya abiria ya Iran kwa makusudi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46580-wamarekani_wakiri_walitungua_ndege_ya_abiria_ya_iran_kwa_makusudi
Afisa wa zamani wa jeshi la Marekani amekiri kwamba jeshi la nchi hiyo liliitungua kwa makusudi ndege ya abiria ya Iran mwaka 1988 kwa shabaha ya kuichochea Iran na kuiingiza katika vita na Marekani.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jul 05, 2018 07:30 UTC
  • Wamarekani wakiri, walitungua ndege ya abiria ya Iran  kwa makusudi

Afisa wa zamani wa jeshi la Marekani amekiri kwamba jeshi la nchi hiyo liliitungua kwa makusudi ndege ya abiria ya Iran mwaka 1988 kwa shabaha ya kuichochea Iran na kuiingiza katika vita na Marekani.

Scott Benett amesema katika kumbukumbu ya siku ya shambulizi la manowari ya kivita ya USS Vincennes dhidi ya ndege ya abiria aina ya Airbus ya shirika la ndege la Iran kwamba, madai kuwa shambulizi hilo lilifanyika kimakosa ni dharau kwa wafanyakazi na Warekani kwa ujumla.

Benett ameongeza kuwa, ni urongo mtupu kudai kuwa shambulizi hilo halikufanyika kwa makusuudi na kwamba Rais wa wakati huo wa Marekani, George W. Bush baba ndiye anayepaswa kubebeshwa lawama la shambulizi hiyo. 

Afisa huyo wa zamani wa jeshi la Marekani amesema George Bush baba na mwana walikuwa watu wapenda vita na wasiofaa. 

Baadhi ya maiti za wahanga wa shambulizi la USS Vincennes

Scott Bennett amesema kuwa raia wa Marekani wanapinga siasa za watawala wa nchi hiyo na sera zao dhidi ya Iran.

Itakumbukwa kuwa tarehe 3 Julai mwaka 1988 manowari ya jeshi la Marekani USS Vincennes ilifyatua makombora mawili dhidi ya ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa safarini kuelekea Imarati na kuua shahidi watu wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo. 66 miongoni mwao walikuwa watoto wadogo wasio na hatia yoyote.