Takwimu: Uingereza imeongeza kuziuzia silaha nchi zinazokiuka haki za binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46867-takwimu_uingereza_imeongeza_kuziuzia_silaha_nchi_zinazokiuka_haki_za_binadamu
Takwimu mpya zilizotolewa zinaonyesha kuwa, Uingereza imeongeza biashara yake ya silaha kwa nchi ambazo zimekuwa zikikiuka haki za binadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2018 22:36 UTC
  • Takwimu: Uingereza imeongeza kuziuzia silaha nchi zinazokiuka haki za binadamu

Takwimu mpya zilizotolewa zinaonyesha kuwa, Uingereza imeongeza biashara yake ya silaha kwa nchi ambazo zimekuwa zikikiuka haki za binadamu.

Takwimu hizo zilizochapishwa na toleo la jana Jumatano na gazeti la Independent la Uingereza inaonyesha kuwa, katika mwaka uliopita wa 2017, serikali ya London iliongeza maradifu kuziuzia silaha zake nchi ambazo ziko katika orodha ya nchi hiyo  ya nchi zinazokiuka haki za binadamu.

Sehemu moja ya ripoti hiyo inasema kuwa, mwaka uliopita, serikali ya Uingereza ilitoa idhini ya kutiwa saini mikataba ya biashara ya silaha yenye thamani ya Pauni bilioni 1.5 katika hali ambayo katika mwaka wa kabla yake thamani ya mikataba ya kuuza silaha nchi hiyo ilikuwa Pauini 820 pekee.

Watoto wa Yemen wamekuwa wakiuawa kwa silaha na Saudia kwa silaha za Uingereza 

Kadhalika ripoti hiyo inabainisha kuwa, mwaka jana Uingereza iliziuzia silaha nchi 18 ambazo kimsingi ziko kkatika faharasa ya nchi zinazokiuka haki za binadamu zikiwemo Saudi Arabia, Bahrain, Israel, Misri na Pakistan.

Ripoti hiyo ianeleza kuwa, serikali ya Theresa May Waziri Mkuu wa Uingereza  imefanya juhudi kubwa kuzipatia siklaha tawala ambazo kwa mujibuu wa London zimekuwa zikikiuka haki za binadamu.

Uingereza na Marekani zimekuwa zikikosolewa sana kutokana na kuendelea kuiuzia Saudi Arabia silaha za aina mbalimbali ambazo zinatumiwa kuua raia wasio na hatia nchini Yemen wakiwemo watoto wadogo.