Jul 30, 2018 08:15 UTC
  • Wakili wa

Wakili aliyekuwa akimtetea Rais wa zamani wa Bosnia katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) katika kesi ya kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Belgrade.

Ripoti zinasema Dragoslav Ognjanović aliyekuwa wakili wa Slobodan Milošević maarufu kama chinjachinja wa Waislamu wa Bosnia Herzegovina aliuawa Jumamosi iliyopita kwa kupigwa risasi mbele ya nyumba yake katika mji mkuu wa Serbia, Belgrade. 

Mtoto wa kiume wa Ognjanović amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mkononi.

Dragoslav Ognjanović alimtetea Milošević katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai huko The Hague nchini Uholanzi alipokuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuua zaidi ya Waislamu elfu nane katika mji wa Srebrenica. 

Slobodan Milošević alitiwa nguvuni mwaka 2001 na kupelekwa katika mahakama ya ICC lakini alifariki dunia akiwa jela kabla ya kumalizika kesi hiyo mwaka 2006. 

Milosevic

Zaidi ya Waislamu elfu nane waliuawa katika hujuma ya Waserbia dhidi ya mji wa Srebrenica na mauaji hayo yanatajwa kuwa makubwa zaidi kufanyika barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. 

Tags