The National Interest: Wademokrati watamlazimisha Trump kujiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47926-the_national_interest_wademokrati_watamlazimisha_trump_kujiuzulu
Jarida la The National Interest la Marekani limeandika kuwa iwapo Wademokrati watadhibiti Kongresi ya nchi hiyo yumkini wakamlazimisha Donald Trump kujiuzulu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 05, 2018 22:30 UTC
  • The National Interest: Wademokrati watamlazimisha Trump kujiuzulu

Jarida la The National Interest la Marekani limeandika kuwa iwapo Wademokrati watadhibiti Kongresi ya nchi hiyo yumkini wakamlazimisha Donald Trump kujiuzulu.

The National Interest limendika makala iliyopewa jina la Zimwi la Tump likisema kuwa, Wademokrati wanaweza kufanya muamala na Donald Trump na kumlazimisha kuondoka Ikulu ya White House, kujiuzulu au kukabiliwa na hasira za kusambaratishwa utajiri na biashara zake na kufungwa jela jamaa zake wa karibu. 

Jarida hilo la Marekani limeongeza kuwa, uchunguzi wa maoni umeonesha kuwa, iwapo Wademokrati watashinda uchaguzi wa Kongresi kutajitokeza msuguano mkubwa unaoweza kumsababishia Trump matatizo mengi ya ndani na nje ya Marekani. 

Limeandika kuwa wiki iliyopita Michael Cohen wakili wa zamani wa Donald Trump alitangaza kuwa, rais huyo wa Marekani alihusika katika njama kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 na ameahidi kutoa maelezo zaidi kuhusu mienendo ya siri ya Trump.

Jarida hilo la Marekani limeandika kuwa, kupatikana na hatia kwa Paul Montfort ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampeni za uchaguzi za Donald Trump na marafiki wengine wa karibu wa Trump ni miongoni mwa mambo yanayomtia kiherehere kiongozi huyo wa Marekani.