Trump aishinikiza Saudia iendelee kurundika silaha za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48489-trump_aishinikiza_saudia_iendelee_kurundika_silaha_za_marekani
Rais Donald Trump wa Marekani ameitaka Saudi Arabia iongeze bajeti yake ya masuala ya kijeshi huku akisisitiza kwamba Washington haipokei kiwango cha fedha ambacho inastahili kupokea kutoka Riyadh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 30, 2018 10:51 UTC
  • Trump aishinikiza Saudia iendelee kurundika silaha za Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani ameitaka Saudi Arabia iongeze bajeti yake ya masuala ya kijeshi huku akisisitiza kwamba Washington haipokei kiwango cha fedha ambacho inastahili kupokea kutoka Riyadh.

Trump ameyasema hayo akihutubia mkutano wa hadhara jimboni West Virginia na kubainisha kuwa, "Nimefanya mazungumzo ya simu na Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudia na nikamwabia bayana kuwa, Riyadh ina matrilioni ya dola na bila sisi nani anajua ni nini kitafanyika? Tunakudhaminieni usalama kikamilifu lakini hatupati kile tunachopaswa kupata mkabala wake."

Huku akizungumza kwa kiburi, kejeli na majivuno, Trump amesema Saudia inapaswa kujigharamia bajeti yake ya kijeshi iwapo inataka kuendelea kudhaminiwa usalama na Washington.

Hivi karibuni, Washington ilikubali kuiuzia Riyadh mifumo 180 ya mizinga yenye thamani ya dola bilioni 1.31 ikiwa ni katika mwendelezo wa Marekani kuiuzia Saudia silaha za mabilioni ya dola.

Trump (kulia) na Mrithi wa Kiti cha Ufamle wa Saudia, Mohammad Bin Salman

Itakumbukwa kuwa akiwa ziarani mjini Riyadh mwaka jana wa 2017, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa, Saudi Arabia itanunua silaha zenye thamani ya dola bilioni 110 kutoka Marekani.

Aidha katika mazungumzo yake hivi majuzi na Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia huko White House, Trump aliitaka Saudia izidishe ununuaji silaha kutoka Marekani.