Taleban: Marekani na serikali ya Afghanistan zinalisaidia genge la Daesh (ISIS)
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49454-taleban_marekani_na_serikali_ya_afghanistan_zinalisaidia_genge_la_daesh_(isis)
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya kundi la Taleban yenye makao yake mjini Qatar amesema kuwa, harakati za makundi ya kigaidi za Daesh (ISIS) nchini Afghanistan, ni mradi wa pamoja wa Washington na serikali ya Kabul.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 12, 2018 01:54 UTC
  • Taleban: Marekani na serikali ya Afghanistan zinalisaidia genge la Daesh (ISIS)

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya kundi la Taleban yenye makao yake mjini Qatar amesema kuwa, harakati za makundi ya kigaidi za Daesh (ISIS) nchini Afghanistan, ni mradi wa pamoja wa Washington na serikali ya Kabul.

Sher Mohammad Abbas Stanikzai ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjino Moscow, Russia na kusisitiza kwamba Daesh ni kundi lisilokuwa na asili yoyote nchini Afghanistan na kwamba wanachama wa kundi hilo wanapata uungaji mkono kutoka Marekani na serikali ya Afghanistan. Aidha Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya kundi la Taleban ameongeza kwamba, miezi michache iliyopita magaidi wa Daesh walizingirwa na wanachama wa Taleban ambapo hata hivyo waliokolewa kwa uingiliaji wa maafisa usalama wa Afghanistan na kwa kutumia helikopta za kijeshi. Stanikzai ameashiria kitendo cha serikali ya Afghanistan cha kukataa kushiriki kikao cha amani cha mjini Moscow, Russia na kudai kwamba serikali ya Kabul haina sifa ya kuwaongoza raia wa nchi hiyo na kwamba Taleban imejiandaa kufanya mazungumzo na vyama na mirengo yote ya kisiasa ya nchi hiyo.

Magaidi wa Kiwahabi wa genge la Daesh (ISIS) wanaosaidiwa na kulindwa na Marekani

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa genge la Taleban amesisitiza kwamba Marekani inatakiwa kuainisha muda wa kuondoka kijeshi nchini Afghanistan na kwamba ili kufikiwa lengo hilo lazima ionyeshe mpango huo kwa jamii ya kimataifa. Kikao cha amani cha mjini Moscow kilifanyika tarehe 8 na 9 za mwezi huu kwa kuwashirikiana wajumbe wa ofisi ya kisiasa ya kundi la Taleban na wawakilishi rasmi na wasio rasmi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Marekani. Katika kikao hicho Taleban ilisisitiza umuhimu wa kuondoka askari wa Marekani huko Afghanistan.