Idadi ya askari wanaojiua nchini Ufaransa yaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53237-idadi_ya_askari_wanaojiua_nchini_ufaransa_yaongezeka
Duru za habari nchini Ufaransa zimeripoti habari ya ongezeko la idadi ya askari wanaojiua nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 03, 2019 00:05 UTC
  • Idadi ya askari wanaojiua nchini Ufaransa yaongezeka

Duru za habari nchini Ufaransa zimeripoti habari ya ongezeko la idadi ya askari wanaojiua nchini humo.

Aidhi Shirika la Habari la Sputnik la Russia limeripoti kwamba tangu mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu zaidi ya askari 30 wamejiua katika nchi hiyo ya Magharibi. Mwaka jana pia idadi ya askari polisi waliojiua katika kipindi kama hicho ilikuwa 35 na kwamba maafisa wengine 33 katika majeshi ya nchi hiyo walijiua pia. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na taasisi ya uchunguzi ya Inserm, kiwango cha askari wanaojiua kati ya askari wa Ufaransa kinafikia asilimia 36 kuliko cha raia wa kawaida nchini humo.

Msongo wa mawazo na matatizo ya kimaisha, chanzo cha askari wa Ufaransa kujiua

Askari wa mwisho kujiua kabla ya ripoti hii kutolewa, ni askari mwenye umri wa miaka 47 aliyejiua tarehe 30 Aprili katika eneo la Réunion nchini Ufaransa. Kabla ya hapo askari mwingine mwenye umri wa miaka 29 alijiua tarehe 28 Aprili mwaka huu katika eneo la Hautes-Alpes, kusini mashariki mwa Ufaransa.