Ilhan Omar: Trump ni mwendawazimu na mtu aliyechanganyikiwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53703-ilhan_omar_trump_ni_mwendawazimu_na_mtu_aliyechanganyikiwa
Mbunge wa Kongresi ya Marekani, Ilhan Omar amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni mwendawazimu, mtu asiye wa kawaida, aliyechanganyikiwa na mwenye huzuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2019 02:26 UTC
  • Ilhan Omar: Trump ni mwendawazimu na mtu aliyechanganyikiwa

Mbunge wa Kongresi ya Marekani, Ilhan Omar amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni mwendawazimu, mtu asiye wa kawaida, aliyechanganyikiwa na mwenye huzuni.

Mbunge huyo wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema hayo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kufafanua kuwa, bwabwaja anazotoa Trump hadharani mara kwa mara zinaonyesha kuwa ana matatizo ya kiakili.

Akizungumza Alkhamisi, Trump alijipiga kifua na kusema kuwa yeye ni mtu razini na mwenye busara na hekima nyingi. Hata hivyo Ilhan Omar akijibu kauli hiyo ya Trump amesema mtu ambaye ana uelewa wa hali ya juu kama anavyojinadi Trump hajitangazi na kujipiga kifua hadharani kila mara.

Huko nyuma, mwakilishi huyo wa Kongresi ya Marekani alimtaja Trump kuwa ni dikteta na kusisitiza kuwa, kuna udharura wa kusailiwa na kutimuliwa kiongozi huyo.

Ilhan Omar (kushoto) na Trump

Kadhalika Spika wa Kongresi ya Marekani Nancy Pelosi ametumia kinaya kujibu matamshi hayo ya majisifu ya Trump kwa kusema, "Mtu mwenye busara nyingi akianza kufanya kazi kama rais wa nchi, nitafurahi kufanya kazi naye katika sekta za miundombinu, biashara na mambo mengine."

Hii ni si mara ya kwanza kwa Trump kujisifu na kujiita mtu mwenye busara na hekima akihutubia wafuasi wake.