Wamarekani wengi wanaamini kwamba, Donald Trump ni mbaguzi wa rangi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55196-wamarekani_wengi_wanaamini_kwamba_donald_trump_ni_mbaguzi_wa_rangi
Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kuwa, zaidi ya nusu ya wananchi wa nchi hiyo wanaamini kwamba, Rais wa nchi hiyo Donald Trump ni mtu mbaguzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 05, 2019 03:47 UTC
  • Wamarekani wengi wanaamini kwamba, Donald Trump ni mbaguzi wa rangi

Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani unaonyesha kuwa, zaidi ya nusu ya wananchi wa nchi hiyo wanaamini kwamba, Rais wa nchi hiyo Donald Trump ni mtu mbaguzi.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonyesha kuwa, asilimia 51 ya wananchi wa Marekani wanaamini kuuwa, Rais Donald Trump ni mbaguzi wa rangi.

Aidha uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac katika jimbo la Kentucky nchini Marekani unaonyesha kuwa asilimia 80 ya raia weusi na 46 ya wazungu walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wanaamini kuwa Rais wa nchi hiyo Donald Trump ni mbaguzi wa rangi. Aidha asilimai 45 ya wananchi wa Marekani wanapinga mtazamo huo. 

Rais wa Marekani hivi karibuni alituma jumbe kadhaa kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo aliwashambulia kwa maneno makali na kuwadhalilisha wawakilishi katika Kongresi ya nchi hiyo ambao si wa wazungu; kitendo kilicholalamikiwa pakubwa na wawakilishi wa chama cha Democrat. 

Rais Donald Trump wa Marekani

Ripoti mbalimbali8 zinasema kuwa, hata kukithiri kwa vitendo vya mauaji ya kutumia risasi nchini Marekani chimbuko lake ni hisia za chuki na ubaguzi.

Matukio mawili ya mauaji ya jana nchini Marekani yameelezwa kuwa, yamechochewa na hisia za chuki na ubaguzi dhidi ya wahamiaji, sera ambazo zimekuwa zikipigiwa debe na Rais wa nchi hiyo Donald Trump.