Trump aagiza kuzidishwa ugaidi wa kiuchumi dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i56105-trump_aagiza_kuzidishwa_ugaidi_wa_kiuchumi_dhidi_ya_iran
Rais wa Marekani amemuagiza Waziri wa Fedha wa nchi hiyo kuweiwekea Iran vikwazo vikuu kufuatia kushindwa siasa za mashinikizo ya juu zaidi za Marekani dhidi ya nchi hii.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 19, 2019 02:37 UTC
  • Trump aagiza kuzidishwa ugaidi wa kiuchumi dhidi ya Iran

Rais wa Marekani amemuagiza Waziri wa Fedha wa nchi hiyo kuweiwekea Iran vikwazo vikuu kufuatia kushindwa siasa za mashinikizo ya juu zaidi za Marekani dhidi ya nchi hii.

Rais Donald Trump aliandika jana katika ukurasa wake wa Twitter kwamba amemuagiza Waziri wa Fedha Steven Mnuchin kuzidisha pakubwa vikwazo dhidi ya Iran. Washington sasa imejikita katika vitendo vya uchochezi baada ya kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ikiwa ni katika kutekeleza siasa zake eti za mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya Iran. 

Steven Mnuchin, Waziri wa Fedha wa Marekani
 

Nayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na subira ya kistratejia katika ajenda yake ya kazi ikiwa ni radiamali yake kwa hatua hizo za Marekani katika muda wa mwaka mmoja; na wakati huo huo imetoa muhula wa kutekeleza majukumu na ahadi zake kwa pande husika katika makubaliano hayo ya nyuklia khususan nchi za Ulaya ambazo inaamini kuwa ndizo zinazopasa kufidia kujitoa huko kwa Marekani ndani ya JCPOA.  

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepunguza uwajibikaji wake katika JCPOA kwa kuchukua hatua tatu hadi sasa katika uwanja huo.