Kuna uwezekano mwanadiplomasia wa serikali ya Trump akatoa ushahidi dhidi yake
https://parstoday.ir/sw/news/world-i56551-kuna_uwezekano_mwanadiplomasia_wa_serikali_ya_trump_akatoa_ushahidi_dhidi_yake
Duru za habari za kuaminika katika Kongresi ya Marekani zimearifu kuwa kuna uwezekano mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Ulaya akatoa ushahidi dhidi ya Trump kuhusu kashfa ya Ukraine Gate.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2019 04:46 UTC
  • Kuna uwezekano mwanadiplomasia wa serikali ya Trump akatoa ushahidi dhidi yake

Duru za habari za kuaminika katika Kongresi ya Marekani zimearifu kuwa kuna uwezekano mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Ulaya akatoa ushahidi dhidi ya Trump kuhusu kashfa ya Ukraine Gate.

Shirika la habari la Reuters leo Ijumaa limezinukuu duru hizo za kuaminika na kuripoti kuwa, Gordon Sandland Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Ulaya kuna uwezekano wiki ijayo akahudhuria katika kamati za uchunguzi za bunge la wawakilishi la Marekani ili kutoa ushahidi. 

Gordon Sandland, Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Ulaya 
 

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani siku kadhaa zilizopita ilimuamuru Sandland kutohudhuria kikao kisicho cha wazi cha siku ya Jumanne katika kamati za uchunguzi za bunge la wawakilishi. 

Ufichuaji uliofanywa na mfanyakazi mmoja wa masuala ya intelijinsia unaonyesha kuwa, katika mazungumzo yake ya simu ya karibuni na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, Rais Donald Trump wa Marekani alimshinikiza kiongozi huyo afanye uchunguzi wa kumfuatilia kisheria Hunter Biden, mwana wa kiume wa Joe Biden, anayetarajiwa kuwa mshindani wake mkuu katika uchaguzi  wa rais wa Marekani wa mwaka 2020.