Nakisi ya bajeti ya Marekani yakaribia dola trilioni moja
https://parstoday.ir/sw/news/world-i56870-nakisi_ya_bajeti_ya_marekani_yakaribia_dola_trilioni_moja
Serikali ya Marekani imemaliza mwaka huu wa kifedha wa 2019 kwa nakisi ya bajeti inayokaribia dola trilioni moja, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi cha nakisi kuwahi kushuhudiwa nchini humo ndani ya miaka saba iliyopita.
(last modified 2026-05-13T14:18:38+00:00 )
Oct 26, 2019 08:32 UTC
  • Nakisi ya bajeti ya Marekani yakaribia dola trilioni moja

Serikali ya Marekani imemaliza mwaka huu wa kifedha wa 2019 kwa nakisi ya bajeti inayokaribia dola trilioni moja, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi cha nakisi kuwahi kushuhudiwa nchini humo ndani ya miaka saba iliyopita.

Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Marekani, nakisi ya bajeti ya nchi hiyo inayodai kuwa kubwa zaidi duniani imefikia dola bilioni 984, ikiwa ni asilimia 4.6 ya mapato jumla ya taifa (GDP).

Hii ni mara ya kwanza tokea mwaka 1980, kwa nakisi hiyo kuongezeka kwa kiwango hicho cha kutisha kwa kipindi cha miaka minne mfululizo. Mwaka jana, nakisi ya bajeti ya nchi hiyo ilikuwa dola bilioni 779.

Wizara ya Hazina ya Taifa ya Marekani

Inaelezwa kuwa hali hiyo inashuhudiwa kutokana na sera mbovu za fedha za utawala wa Donald Trump. Nakisi hiyo ya bajeti ya Marekani imeshuhudiwa pia mwaka huu kwa sababu ya kuongezeka madeni ya serikali ya Washington ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita. 

Mwezi Februari mwaka huu, Wizara ya Fedha ya Marekani iliripoti kuwa, nchi hiyo inadaiwa dola trilioni 22, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.