Kuna watu milioni 38 masikini nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57034-kuna_watu_milioni_38_masikini_nchini_marekani
Raia wa Marekani wasiopungua milioni 38, wakiwemo watoto milioni 12 wanaishi katika umasikini wa kupindukia katika nchi hiyo ambayo ina utajiri mkubwa na Pato Ghafi la Taifa la juu zaidi duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2019 09:15 UTC
  • Kuna watu milioni 38 masikini nchini Marekani

Raia wa Marekani wasiopungua milioni 38, wakiwemo watoto milioni 12 wanaishi katika umasikini wa kupindukia katika nchi hiyo ambayo ina utajiri mkubwa na Pato Ghafi la Taifa la juu zaidi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Televisheni ya Al Jazeera, wanawake asilimia 9.12 na wanaume asilimia 6.10  yaani takribani raia milioni 38 wa Marekani wanaishi katika umasikini wa kupindukia. Taarifa hiyo imeongeza kuwa idadi kubwa ya watu masikini nchini Marekani ni kutoka jamii za waliowachache hasa Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Marekani, karibu watoto milioni 12 nchini humo wanaishi chini ya mstari wa umasikini.

Ripoti hiyo imedokeza kuwa majimbo ya Virginia Magharibi, Mississippi na Arkansas yanaongoza katika umasikini duniani.

Maandamano ya kupinga umasikini Marekani

Hali kadhalika Wamarekani ambao mwaka 2018 hawakua na bima ya afya walikuwa zaidi ya milioni 30 huku watu zaidi ya nusu milioni Marekani wakiwa hawana nyumba na hivyo kulazimika kulala barabarani.