Akthari ya Wamarekani hawaungi mkono namna Trump anavyoamiliana na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i58471-akthari_ya_wamarekani_hawaungi_mkono_namna_trump_anavyoamiliana_na_iran
Utafiti mpya wa maoni uliofanywa na shirika la Ipsos likishirikiana na kanali ya televisheni ya ABC News ya Marekani unaonyesha kuwa, aghalabu ya wananchi wa Marekani hawaungi mkono sera ghalati za Rais Donald Trump dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 12, 2020 21:07 UTC
  • Akthari ya Wamarekani hawaungi mkono namna Trump anavyoamiliana na Iran

Utafiti mpya wa maoni uliofanywa na shirika la Ipsos likishirikiana na kanali ya televisheni ya ABC News ya Marekani unaonyesha kuwa, aghalabu ya wananchi wa Marekani hawaungi mkono sera ghalati za Rais Donald Trump dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 57 ya Wamarekani wanahisi kuwa sera na mienendo ya Trump dhidi ya Iran haijawa na matokeo mengine ghairi ya kushadidisha taharuki na uhasama baina ya Washington na Tehran.

Aidha zaidi ya nusu ya wananchi wa Marekani hawaungi mkono kauli ya Trump kwamba Wamarekani wapo salama zaidi hivi sasa baada ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

Baada ya Trump kutoa agizo la kutekelezwa jinai hiyo ambayo inaendelea kulaani katika pembe mbalimbali za dunia, alidai kuwa Marekani, eneo la Asia Magharibi na dunia kwa ujumla hivi sasa ni salama zaidi.

Maandamano ya kupinga sera za kupenda vita za Trump

Hii ni katika hali ambayo, siku chache baada ya mauaji hayo ya Jenerali Soleimani, wanaharakati mbalimbali wa kupinga vita walifanya maandamano katika maeneo tofauti ya Marekani wakilaani uchu wa vita wa utawala wa Trump.

Kadhalika walilaani vikali hatua ya Washington ya kutuma askari elfu tatu zaidi katika eneo la Asia Magharibi baada ya ukatili huo uliofanywa kwa amri ya Trump karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege mjini Baghdad nchini Iraq mapema mwezi huu.