Ujerumani: Marekani imeshindwa katika makabiliano yake na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i58620-ujerumani_marekani_imeshindwa_katika_makabiliano_yake_na_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amekosoa siasa za uhasama za White House dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu ya Washington dhidi ya Tehran hazina natija.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 19, 2020 23:26 UTC
  • Heiko Maas
    Heiko Maas

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amekosoa siasa za uhasama za White House dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu ya Washington dhidi ya Tehran hazina natija.

Akihojiwa na gazeti la Ujerumani la Bild, Heiko Maas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani huku akikosoa siasa za mashinikizo ya juu kabisa ya Washington dhidi ya Tehran, amesema kwamba siasa mbovu za vitisho na operesheni za kijeshi za Marekani hazijabadilisha lolote katika mienendo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Heiko Maas amekosoa waziwazi siasa zinazotekelezwa na serikali ya Marekani dhidi ya Iran na kutahadharisha juu ya uwezekano wa kuenea mgogoro katika eneo zima la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Katika mahojiano hayo, Heiko Maas kwa mara nyingine ametetea mazungumzo ya nyuklia kati ya madola sita makuu ya dunia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mashuhuri kama JCPOA bila kuashiria uvunjaji wa Troika ya Ulaya (Ujerumani, Ufaransa na Uingereza) wa ahadi zake za JCPOA huku akiitaka Iran iendelee kutekeleza uwajibikaji wake wa mapatano hayo. 

Heiko Maas

Baada ya kujiondoa katika mapatano hayo ya kimataifa tarehe 8 mwezi Mei 2018, Marekani ilianza kutekeleza siasa za kutoa mashinikizo ya pande zote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ni zaidi ya miezi 9 sasa ambapo serikali ya Donald Trump imefutilia mbali msamaha iliokuwa imeutoa kwa nchi za kigeni kununua mafuta ya Iran kwa lengo eti la kusimamisha kabisa uuzwaji nje wa mafuta ya Iran katika soko la kimataifa, jambo ambalo imeshindwa kabisa kulifikia hadi sasa, licha ya kutoa vitisho vya kila aina katika uwanja huo.

Nchi nyingi zikiwemo za China, India, Iraq, Russia na Uturuki zimesisitiza kuwa zitaendelea kununua mafuta ya Iran licha ya vikwazo vya upande mmoja vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Tehran.