Apr 03, 2021 11:57 UTC
  • 7 waaga dunia UK kwa kuganda damu baada ya kupigwa chanjo ya AstraZeneca

Wakala wa Kudhibiti Madawa Uingereza (MHRA) umesema miongoni mwa watu 30 waliopaata matatizo ya kuganda damu baada ya kupigwa chanjo ya AstraZeneca, saba wameaga dunia.

Taarifa ya leo Jumamosi ya wakala huo imesema, hadi kufikia Machi 24, ulikuwa umepokea kesi 30 za watu walioachanjwa kukumbwa na matatizo ya kuganda kwa damu, na saba miongoni mwao wamefariki dunia.

Hata hivyo Wakala wa Kudhibiti Madawa Uingereza unasisitiza kuwa, manufaa ya chanjo hiyo yangali na uzito ikilinganishwa na madhara yake.

Uholanzi hapo jana ilijiunga na orodha ya nchi za Ulaya zilizotangaza kusimamisha utoaji wa chanjo ya AstraZeneca kwa watu wenye chini ya umri wa miaka 60, baada ya kuripoti kesi tano za madhara ya chanjo hiyo kwa wanawake walio na umri kati ya miaka 25 na 60, ambapo mmoja wao aliaga dunia.

Mwezi uliopita wa Machi, nchi ya sita za Ulaya zilisimamisha matumizi ya chanjo hiyo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 ya AstraZeneca kutokana na madhara yake kwa damu za watu waliopigwa chanjo hiyo.

Mgonjwa akipimwa joto la mwili

Matokeo ya uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni yanaonesha kuwa, idadi kubwa ya Wazungu wa Ulaya hawana imani na wamekatishwa tamaa na chanjo ya Corona ya AstraZeneca inayozalishwa Uingereza.

Shirika la Afya Duniani WHO linatazamiwa Aprili 7 kutoa taarifa kuhusu chanjo hiyo, ingawaje huko nyuma ilisisitiza kuwa, madhara ya chanjo hiyo si makubwa ukilinaganisha na manufaa yake.

Tags