Jan 25, 2022 11:13 UTC
  • Jeremy Rimbaud akiwa mikononi mwa polisi
    Jeremy Rimbaud akiwa mikononi mwa polisi

Polisi wa Ufaransa wanasema kuwa wamemkamata mwanajeshi mwenye historia ya kufanya uhalifu kabla ya kumuwinda ajuza mmoja kwa ajili ya kula nyama yake.

Ripoti zinasema kuwa, Jeremy Rimbaud, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa, alimshambulia ajuza mwenye umri wa miaka 73 baada ya kutoroka hospitalini katika mji wa kusini-magharibi mwa Ufaransa wa Toulouse kwa shabaha ya kutaka kula nyama yake, lakini hatimaye alikamatwa baada ya upekuzi wa kina wa polisi na askari usalama.

Jeremy Rimbaud, mwenye umri wa miaka 34 ambaye alihudumu kama mwanajeshi nchini Afghanistan, alimshika mhanga wake wa hivi karibuni ambaye hakutajwa jina kwenye mji wa Toulouse siku ya Jumatano iliyopita.

Mwaka 2013 Rimbaud, ambaye ana historia ya kutenda uhalifu, alimuua mkulima mmoja na kula nyama yake.

Jeremy Rimbaud akiwa mikononi mwa polisi

Kabla ya kukamatwa kwake, polisi walikuwa wamesambaza picha za mla nyama za watu, na kuwatahadharisha raia hususan wazee, wasiondoke nyumbani peke yao. Tangazo hilo lilizusha wimbi la hofu na woga katika eneo la Pyrenees nchini Ufaransa.

Jeremy Rimbaud alihudumu katika jeshi la nchi kavu la Ufaransa kwa miaka mitano na alikuwa katika kikosi cha jeshi la Ufaransa kilichotumwa Afghanistan kupambana na Taliban kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 2010.

Habari ya askari mla nyama za watu nchini Ufaransa sasa inazungumzwa zaidi kwenye vyombo vya habari na magazeti kuliko habari za maambukizi ya corona na uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Tags