Azma ya Tunisia ya kujiunga na Jumuiya Ushirikiano ya Shanghai (SCO)
(last modified 2023-04-09T08:00:19+00:00 )
Apr 09, 2023 08:00 UTC
  • Azma ya Tunisia ya kujiunga na Jumuiya Ushirikiano ya Shanghai (SCO)

Msemaji wa chama cha Harakati ya Julai 25 chenye mfungamano na Rais wa Tunisia amesema kuwa nchi hiyo inajipanga kujiunga na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

Mahmoud Ben Mabrouk ametangaza kuwa Tunisia inafanya jitihada kubwa kwa ajili ya kujiunga na jumuiya ya Shanghai. Tunisia inafanya jitihada za kujiunga na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai katika hali ambayo mazungumzo kati ya nchi hiyo na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) yamegonga mwamba.  

Mahmoud Ben Mabrouk,  msemaji wa Harakati ya Julai 25 ya Tunisia 

Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai iliundwa mwaka 1996 kwa ubunifu wa China, Russia, Qazakistan, Qirqizistan na Tajikistan  lengo likiwa ni kuleta mlingano mkabala wa satwa ya Marekani na Nato katika eneo. Uzbekistan ilijiunga pia na jumuiya hiyo baada ya kupita miaka kadhaa tangu kuasisiwa kwake. 

Mbali na wanachama wake wa asili, Mongolia ilijiunga na jumuiya  hiyo mwaka 2004 na Iran, Pakistani, India na Afghanistan mwaka 2005 na kisha Belarus kama nchi wanachama waangalizi. Mwaka 2017 India na Pakistan zilipata hadhi ya wanachama kamili wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Jumuiya ya Shanghai  ilikubali Iran kuwa mwanachama wake kufuatia ziara iliyofanywa Septemba 17 mwaka 2021 na Rais Sayyid Ebrahim Rais wa Iran huko Dushanbe mji mkuu wa Tajikistan na tarehe 17 Septemba mwaka jana Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikapata unachama rasmi ndani ya jumuiya hiyo.

Tags