Jul 17, 2018 02:58 UTC
  • Jumanne tarehe 17 Julai 2018

Leo ni Jumanne tarehe 03 Dhulqaada 1439 Hijria sawa na Julai 17, 2018.

Siku kama ya leo miaka 105 iliyopita Profesa Roger Garaudy, mwanafalsafa na mwanafikra wa Ufaransa alizaliwa huko katika mji wa Marseille. Garaudy alipata shahada ya daraja ya udaktari katika taaluma tatu za masomo ya falsafa, fasihi na utamaduni. Roger Garaudy alifungwa jela katika kambi ya mateka wa kivita wa Ujerumani tangu mwaka 1940 hadi 1943 kutokana na mapambano yake dhidi ya ufashisti wa Adolph Hitler wakati Ufaransa ilipokaliwa kwa mabavu na Ujerumani. Profesa Garaudy alikuwa mwanachama wa chama cha Kikomonisti cha Ufaransa kwa miaka 36 na pia mwanachama wa kamati kuu ya chama hicho kwa miaka 25. Hata hivyo mitazamo ya kikomunisti na kiliberali haikuweza kukata kiu ya kutafuta ukweli ya msomi huyo wa Ufaransa na hatimaye alikubali dini ya tukufu ya Uislamu baada ya kufanya utafiti mkubwa. Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran mwaka 1979 ulikuwa na taathira kubwa katika mitazamo ya Profesa Roger Garaudy.

Faustin-Archange Touadéra

Miaka 50 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo chama cha Baath cha Iraq kilichukua hatamu za uongozi kupitia mapinduzi yaliyoongozwa na Ahmad Hassan al Bakr na kumpindua Rais Abdulrahman Aarif. Baada ya kuchukua madaraka chama cha Baath, Saddam Hussein ambaye alikuwa kiongozi nambari mbili wa chama hicho alianza kuwauwa wapinzani wake nchini Iraq na vikosi vya usalama na vya jeshi la nchi hiyo pia vikaanzisha hujuma kali dhidi ya wapinzani wa Kikurdi, wazalendo, wanaharakati wa Kiislamu na hata Wakomonisti.

Ahmad Hassan al Bakr

Na tarehe 26 Tir miaka 38 iliyopita Baraza la kwanza la Kulinda Katiba ya Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran lilianza rasmi kazi zake. Kwa mujibu wa kifungu nambari 91 cha Katibu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa lengo la kulinda sheria za Kiislamu na kuhakikisha kwamba sheria zinazopasishwa na Bunge hazipingani na dini ya Uislamu na Katiba, kuliundwa baraza lililopewa jina la Baraza la Kulinda Katiba. Baraza hilo lina wanazuoni sita wa fiqhi na sheria za Kiislamu wanaoteuliwa na Kiongozi Mkuu wa Iran na wataalamu 6 wa sheria ambao huarifishwa bungeni na kupigiwa kura baada ya kuteuliwa na Idara ya Vyombo vya Mahakama. Wadhifa mkubwa zaidi wa baraza hilo ni kuhakikisha kwamba, sheria zinazopasishwa na Bunge hazipingani na sheria za Kiislamu na Katiba, kufasiri Katiba na kusimamia chaguzi mbalimbali hapa nchini.