Aug 13, 2019 02:43 UTC
  • Jumanne tarehe 13 Agosti 2019

Leo ni Jumanne tarehe 11 Dhulhija 1440 Hijria sawa na Agosti 13 mwaka 2019.

Siku kama ya leo miaka 156 iliyopita aliaga dunia Frederick Eugene Delacroix, mchoraji maarufu wa Ufaransa. Eugene Delacroix alirithi kipaji cha sanaa ya uchoraji kutoka kwa mama yake. Baada ya kupoteza wazazi wake wawili akiwa kijana mdogo na kujikuta akiishi maisha magumu sana ya umasikini, aliamua kufanya juhudi kubwa katika kujiendeleza na fani yake uchoraji. Baadaye alianza kufanya maonyesho ya sanaa hiyo katika ukumbi wa jiji la Paris. Katika kipindi hicho baadhi ya watu walikuwa wakimfanyia maskhara na kumkebehi, hata hivyo hakuvunjika moyo na hatimaye kazi zake zilikuwa na taathira. Alipata umashuhuri katika kipindi kifupi na kazi zake zikapokewa sana katika jamii.

Frederick Eugene Delacroix,

Siku kama ya leo miaka 120, yaani tarehe 13 Agosti miaka 115 iliyopita, alizaliwa Alfred Hitchcock mtengeneza filamu mashuhuri wa Kiingereza. Alionesha kazi yake ya kwanza mwaka 1920 na baadaye akaanza kujihusisha na uongozaji filamu. Filamu zake za kuogopesha na za kusisimua zilikuwa mashuhuri mno katika zama hizo. Filamu hizo zilimfanya awe mashuhuri kwa jina la the Master of Suspense. Miongoni mwa filamu zake ni The Man Who Knew Too Much na Young and Innocent. Alfred Hitchcock aliaga dunia tarehe 28 Aprili 1980.

Alfred Hitchcock

Siku kama ya leo miaka 109 iliyopita, aliaga dunia Florence Nightingale, mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa huko nchini Italia, akiwa na umri wa miaka 90. Nightingale alizaliwa tarehe 12 Mei 1820 nchini Italia. Aliishi kipindi kirefu cha ujana wake nchini Uingereza. Akiwa kijana alifanya juhudi kubwa katika kuwasaidia watu, suala ambalo alilipa umuhimu mkubwa kuliko kitu kingine chochote na hatimaye alisabilia maisha yake kwa amjili ya kuuguza wagonjwa. Bi, Florence Nightingale alikuwa muuguzi na mwanahesabati mashuhuri wa Uingereza. Alipewa lakabu ya ''Mwanamke Mwenye Taa Mkononi' kutokana na uvumilivu wake mkubwa na kujinyima usingizi kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa nyakati za usiku. Alifanya juhudi kubwa pia kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika hospitali nyingi nchini Uingereza. Kazi hiyo aliyoifanya kwa miaka mingi bila kuchoka ilimdhoofisha sana kimwili kwa kadiri kwamba alikuwa kipofu mwishoni mwa umri wake na hatimaye aliaga dunia tarehe 13 Agosti 1910.

Florence Nightingale

Miaka 96 iliyopita katika siku kama ya leo yaani tarehe 11 Mfunguo Tatu Dhul-Hijja alifariki dunia Ayatullah Mirza Jawad Malaki Tabrizi ustadhi mkubwa wa akhlaqi, msomi na arif. Alizaliwa katika mji wa Tabriz moja ya miji ya Iran na baada ya kukamilisha masomo yake ya msingi na ya kati alielekea katika Chuo Kikuu cha Kidini cha Najaf nchini Iraq. Akiwa huko alihudhuria darsa za maustadhi mahiri katika zama hizo kama Haji Agha Reza Hamadani, Akhund Khorasani, Muhaddith Nuri na Akhund Hamedani. Mwanazuoni huyo mbali na kufundisha na kulea wanafunzi wengi hakuwa nyuma pia katika taaluma ya uandishi wa vitabu. Asraru Salat, al-Muraqabaat na A'amalu al Sunna ni baadhi tu ya vitabu vya Ayatullah Mirza Jawad Maliki Tabrizi.

Ayatullah Mirza Jawad Malaki Tabrizi

Siku kama ya leo miaka 49 iliyopita, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilijikomboa na kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mfaransa. Ilikuwa katikati ya karne ya 19 wakati nchi hiyo iliyokuwa ikijulikana hapo kabla kwa jina la Ubangi-Shari, ilipounganishwa na makoloni ya Ufaransa barani Afrika. Hata hivyo mwaka 1958, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilijipatia mamlaka ya ndani na miaka miwili baadaye yaani mwaka 1960, ikajikomboa na kupata uhuru kamili. 

Tags