Jul 13, 2023 02:15 UTC
  • Alkhamisi, tarehe 13 Julai, 2023

Leo ni Alkhamisi tarehe 24 Dhulhija 1444 Hijria sawa na Julai 13, mwaka 2023.

Siku kama ya leo miaka 1959 iliyopita, moto mkubwa ulitokea huko Roma mji mkuu wa utawala wa kifalme wa Roma. Sehemu kubwa ya mji wa kihistoria na mkongwe wa Roma iliungua na wakazi wengi wa mji huo walipoteza maisha yao kutokana na moto huo. Moto huo ulikuwa kisingizio tosha kwa Nuren mtawala mmwagadamu wa Kirumi ambaye aliwauwa kwa umati watu zaidi ya laki moja na baadaye kuwatuhumu Wakristo kuwa ndio walioanzisha moto huo. 

Siku kama ya leo miaka 1435 iliyopita kwa mujibu wa nukuu mashuhuri ya kihistoria Mtume Muhammad (SAW) akiwa pamoja na binti yake Bibi Fatima (AS), mkwewe Ali bin Abi Twalib (AS) na wajukuu wake wawili Hassan na Hussain (AS) waliondoka mjini Madina kwenda kufanya mdahalo na viongozi wa Wakristo wa eneo la Najran juu ya dini ya kweli. Tukio hilo linaelezwa na Mwenyezi Mungu SW katika aya za 60 na 61 za sura ya Aal Imran. Wakati viongozi wa Najran walipoona Mtume amekuja katika mdahalo huo akiwa na watu wanne tu wa Nyumba yake tukufu walipigwa na mshangao na kuelewa kwamba, dua ya mtukufu huyo ya laana kwa atakayesema uongo itakubaliwa. Katika hali hiyo askofu wa Najran alisema: "Ninaziona nyuso ambazo iwapo zitamuomba Mwenyezi Mungu aung'oe mlima mkubwa zaidi mahala pake basi dua yao itajibiwa papo hapo. Kwa msingi huo si sahihi kufanya mdahalo na watu hawa watakatifu kwani yumkini kizazi chetu chote kikaangamia." Baada ya hapo askofu huyo wa Najran alimuomba Mtume (SAW) kufanya suluhu na kusamehe. Tukio hilo la kihistoria lilidhihirisha haki na ukweli wa dini tukufu ya Kiislamu na utukufu na nafasi aali ya Ahlubait wa Mtume Muhammad (SAW). 

Miaka 623 iliyopita katika siku kama ya leo, liliundwa jeshi la kale zaidi duniani nchini Uswisi. Jeshi hilo la kale zaidi duniani hadi hii leo limebakia kama lilivyokuwa na hata mavazi ya wanajeshi wake hayajabadilika. Idadi ya wanajeshi wa jeshi hilo dogo lakini lenye nidhamu kubwa ni watu 83. Jeshi hilo ambalo wanachama wake daima huwa raia wa Uswisi, liliundwa kwa ajili ya kulinda viongozi wa Kikatoliki wa wakati huo na hii leo baada ya kupita zaidi ya miaka zaidi ya 600 tangu liundwe, jeshi hilo lina jukumu la kumlinda Papa wa Kanisa Katoliki huko Vatican. 

Katika siku kama ya leo miaka 252 iliyopita, baharia na nahodha mashuhuri wa Kiingereza aliyejulikana kwa jina la James Cook alikamilisha safari yake ya kitafiti na kielimu ya kuelekea The Great Southern Continent. Safari hiyo ilikuwa imeanza tarehe 26 Julai mwaka 1768. Safari hiyo ndefu iliishirikisha pia timu ya watalaamu wa elimu ya Sayansi Asilia au Natural Science kwa kimombo. Wataalamu hao walikuwa na nia ya kufanya utafiti wa kielimu kuhusiana na mimea pamoja na viumbe wanaopatikana katika maeneo hayo.

James Cook

Miaka 32 iliyopita katika siku kama ya leo ya tarehe 22 Tir 1370, Hijria Shamsia aliaga dunia, Allamah Sayyid Tahir Sayyidzadeh Hashemi, mmoja wa wanafikra wa Kiirani. Aliaga dunia katika viunga vya mjii wa Kerman ulioko magharibi mwa Iran. Katika kipindi chote cha maisha yake, Sayyyidzadeh Hashemi alijishughulisha na uenezaji na usambazaji wa maarifa ya Kiislamu kupitia kufundisha na kulea wanafunzi wa masomo ya dini, kutoa mawaidha na kuandika vita.  Kwa hakika alimu huyu ametoa huduma kubwa katika uwanja huu. Allamah Sayyidzadeh Hashemi alikuwa ametabahari pia katika fani ya hati. Alimu huyo alikuwa akizifahamu vizuri na kikamilifu lugha za Kiarabu, Kifarsi na Kikurdi na alikuwa mahiri pia katika utunzi wa mashairi na ameacha athari nyingi katika uwanja huo kwa lugha hizo tatu. 

Allamah Sayyid Tahir Sayyidzadeh Hashemi

Na tarehe 13 Julai inayosadifiana na Jumamosi ya leo ni siku ya kumbukumbu ya  Romania kujipatia uhuru kutoka kwa Utawala wa Othmania. Kijiografia Romania ipo kusini mashariki mwa Ulaya na magharibi mwa Bahari Nyeusi. Romania ina zaidi ya wakazi milioni 22 na dini rasmi ya nchi hiyo ni Ukristo na madhehebu ya Orthodox ndiyo yenye wafuasi wengi. Nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa Othmania kuanzia karne yay 15. Hata hivyo mwaka 1877 Romania iliungana na Russia katika vita dhidi ya utawala wa Othmania. Hatimaye katika siku kama ya leo Romalia ikajipatia uhuru na miaka mitatu baadaye ikawa imepata uhuru kamili.

 

Tags