May 27, 2021 07:50 UTC
  • Baada ya kudhalilishwa Gaza, Israel sasa yaitishia vita Lebanon

Baada ya kudhalilishwa na kushindwa vibaya na kambi ya muqawama katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, utawala wa Kizayuni wa Israel sasa unatishia kuishambulia kijeshi Lebanon.

Waziri wa Vita wa Israel, Benny Gantz katika hotuba hapo jana alisema: Iwapo shambulio lolote litatokea upande wa kaskazini, Lebanon itatikisika. 

Amesema utawala huo utaishambulia Lebanon kwa nguvu zaidi kuliko Gaza, na eti nyumba zinazotumiwa kuficha silaha na magaidi zitageuzwa kuwa vifusi.

Tel Aviv imetoa vitisho hivyo muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah kuuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa hujuma dhidi ya maeneo matukufu katika mji wa Quds (Jerusalem) inaweza kupelekea kuibuka vita vya kieneo na kuangamizwa utawala huo wa Kizayuni.

Makombora na maroketi ya HAMAS dhidi ya Israel

Amesema pale maeneo matakatifu ya Waislamu na Waktristo yanapokabiliwa na hatari, harakati za muqawama haziwezi kukaa kimya na kuwa watazamaji.

Israel ilianzisha vita dhidi ya raia wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Ghaza tangu tarehe 10 mwezi huu wa Mei; na kumalizika tarehe 21 kufuatia ombi la baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni na upatanishi wa baadhi ya pande ajinabi baada ya kushindwa jeshi la utawala huo kukabiliana na wanamuqawama wa Palestina. 

Tags