Daesh 40 wauawa Sinai, Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1000-daesh_40_wauawa_sinai_misri
wapiganaji zaidi ya 40 wa kundi la kigaidi la Daesh wameuawa huko kaskazini mwa Sinai nchini Misri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2016 00:23 UTC
  • Daesh 40 wauawa Sinai, Misri

wapiganaji zaidi ya 40 wa kundi la kigaidi la Daesh wameuawa huko kaskazini mwa Sinai nchini Misri.

Magaidi hao waliuawa jana baada ya helikopta za jeshi la Misri kushambulia maficho yao Sinai Kaskazini.

Jeshi la Misri limetangaza kuwa operesheni hiyo imefanyika baada ya magaidi wa kundi la Daesh kulenga gari moja la jeshi kusini mwa mji wa Sheikh Zuwaid na kuongeza kuwa, magaidi wengi wameangamizwa katika shambulio hilo.

Shambulizi lililofanywa na magaidi wa Daesh dhidi ya gari hilo la jeshi la Misri lilisababisha vifo vya watu wanne.

Septemba mwaka 2013 Jeshi la Misri lilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi la kupambana na wapiganaji wa kundi la Daesh katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo hususan katika peninsula ya Sinai.