Human Rights Watch: Tunisia inawadhalilisha pakubwa wahamiaji weusi wa Kiafrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i100120-human_rights_watch_tunisia_inawadhalilisha_pakubwa_wahamiaji_weusi_wa_kiafrika
Shirika la Human Rights Watch limeeleza kuwa askari usalama wa Tunisia wamefanya unyanyasaji mkubwa dhidi ya wahamiaji weusi wa Kiafrika na limetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kusimamisha ufadhili wa kudhibiti uhamiaji nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 20, 2023 07:56 UTC
  • Human Rights Watch: Tunisia inawadhalilisha pakubwa wahamiaji weusi wa Kiafrika

Shirika la Human Rights Watch limeeleza kuwa askari usalama wa Tunisia wamefanya unyanyasaji mkubwa dhidi ya wahamiaji weusi wa Kiafrika na limetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kusimamisha ufadhili wa kudhibiti uhamiaji nchini humo.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini New York, Marekani, limesema kuwa tangu mwezi Machi mwaka huu limewahoji wahajiri na raia wanaotafuta hifadhi zaidi ya 20 ambapo aghalabu yao waliweka wazi unyanyasaji na ukiukaji wa haki za binadamu waliopitia wakiwa mikononi mwa mamlaka husika za Tunisia.  

Wahajiri saba kati ya 20 waliohojiwa na HRW walikuwa miongoni mwa wahajiri weusi wa Kiafrika 12,00 ambao mwezi huu walifukuzwa au kulazimishwa na askari usalama wa Tunisia kuelekea maeneo ya  jangwani ya nchi hiyo inayopakana na Libya na Algeria.

Ripota wa shirika la habari la AFP Jumapili iliyopita aliripoti kuwa walinzi wa mpakani wa Libya wameokoa makumi ya wahajiri wa Kiafrika ambao walikuwa hoi huku wakiwa wameishiwa maji mwilini. Wahajiri hao walisema kuwa mamlaka husika za Tunisia ndizo zilizowateleleza katika maeneo hayo ya jangwani. 

Taarifa hizi zimetolewa kufuatia ushahidi uliowasilishwa na mashirika yasiyo ya kiserikali na mashahidi kwa AFP siku chache baada ya mamia ya wahajiri weusi wa kiafrika kufukuzwa katika mji wa bandari wa Sfax mapema mwezi huu. Jumapili iliyopita Umoja wa Ulaya na Tunisia zilisaini hati ya maelewano kwa ajili ya ushirikiano wa kimkakati na mkubwa kuhusu masuala  uhamiaji usio wa kawaida, maendeleo ya kiuchumi na nishati jadidika. 

Tunisia na ukandamizaji dhidi ya wahajiri wa Kiafrika 

Shirika la Human Rigths Watch limeongeza kuwa dhulma nyingi ilizoripoti zimejiri baada ya Rais Kais Saied wa Tunisia mwezi Februari mwaka huu kuyatuhumu makundi ya wahamiaji kutoka katika chini za chini ya Jangwa la Sahara kuwa yanasababisha machafuko nchini humo ili kubadili muundo wa kidemografia wa Tunisia.