Jul 03, 2016 13:26 UTC
  • Silaha za waasi zanaswa kusini mashariki mwa Kongo DR

Duru za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasa ya Kongo zimearifu habari ya kukamatwa idadi kadhaa ya silaha zilizokuwa zikimilikiwa na waasi huko kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Duru hizo zimeripoti kuwa kamisheni ya kudhibiti silaha ya Kongo imekamata silaha 34 za waasi kufuatia oparesheni iliyofanywa kwa siku tatu katika vijiji vya eneo la Mitwaba katika mkoa wa Haut -Katanga kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Duru za kijeshi za Kongo zimetangaza kuwa oparesheni hiyo imetekelezwa lengo likiwa ni kuzuia ubebaji silaha katika mkoa wa Haut-Katanga ambao umekumbwa na machafuko kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi wa Mai-Mai.

Ripoti zinasema kuwa oparesheni hiyo ya ukusanyaji silaha za waasi huko kusini mashariki mwa Kongo itaendelea hadi zitakapokusanywa silaha zaidi ya elfu tatu kutoka kwa waasi katika mkoa mzima wa Haut-Katanga.

Tags