Katibu Mkuu wa Hizbullah asisitiza kuendelezwa uungaji mkono kwa watu wa Palestina
-
Sayyid Hassan Nasrullah
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, mapambano ya kuunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza yataendelea hadi kutimizwa malengo ya wananchi wa Palestina na ya wanamapambano wa ukombozi.
Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisisitiza jana katika hotuba yake huko Beirut, mji mkuu wa Lebanon kwa mnasaba wa mwezi wa Muharram kwamba, Muqawama wa Lebanon ambao ulianza shughuli zake Oktoba 8 mwaka jana kwa ajili ya kuwaunga mkono watu madhulumu wa Palestina mkabala wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni, utaendelea hadi kufikiwa lengo la makundi yote ya ukombozii na hakuna kurudi nyuma.
Sayyid Nasrullah ameongeza kuwa: Harakati na makundi yote yamapambano ya uukombozi yanayoiunga mkono Gaza huko Lebanon, Iraq na Yemen na waungaji mkono wakuu wa kisiasa wa Gaza katika eneo hili ni taswira yenye kutia furaha.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameeleza kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ni jeshi lisilo na maadili zaidi duniani na kwamba kwa miezi kadhaa sasa hakuna msaada wowote ulioingia Ukanda wa Gaza, na eneo hilo linakabiliwa na hatari ya njaa na magonjwa.