Wanawake na watoto, wahanga wakuu wa migogoro ya Afrika
(last modified Sat, 13 Feb 2016 15:22:24 GMT )
Feb 13, 2016 15:22 UTC
  • Wanawake na watoto, wahanga wakuu wa migogoro ya Afrika

Wanawake na watoto wametajwa kuwa ndiyo wahanga wakuu wa migogoro inayozikumba nchi kadhaa za Afrika.

Ripoti zinaonesha kuwa, machafuko yanayotokeo katika nchi kama Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Somalia na Sudan Kusini yanawaathiri zaidi raia hususan na wanawake na watoto wadogo. Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Afrika, Soyata Maiga amesema kuwa wanawake na watoto ndio waathirika wa kwanza wa migogoro wa ndani katika nchi za Afrika na kwamba mbali na kupigwa, wanawanake katika nchi hizo za Kiafrika wanasumbuliwa na ukatili wa kubakwa na kunajisiwa na kwamba kwa kawaida wahusika wa vitendo hivyo viovu huwa hawachukuliwi hatua yoyote.

Maiga ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanya uhakiki na kutayarisha ripoti za kutetea haki za wanawake, ameeleza matumaini ya kuhitimishwa migogoro wa ndani katika nchi za Afrika kwa kuchukuliwa maamuzi madhubuti.

Tags