Radiamali ya kiongozi wa Boko Haram kufuatia kuteuliwa kiongozi mpya na Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12604-radiamali_ya_kiongozi_wa_boko_haram_kufuatia_kuteuliwa_kiongozi_mpya_na_daesh
Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram la nchini Nigeria amesema kuwa wanachama wa kundi hilo hawaafiki kuteuliwa mjumbe yoyote kutoka kundi la Daesh kuwa kiongozi wao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 04, 2016 15:06 UTC
  • Radiamali ya kiongozi wa Boko Haram kufuatia kuteuliwa kiongozi mpya na Daesh

Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram la nchini Nigeria amesema kuwa wanachama wa kundi hilo hawaafiki kuteuliwa mjumbe yoyote kutoka kundi la Daesh kuwa kiongozi wao.

Habari kutoka Kano zinasema kuwa Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram leo ametuma ujumbe wa sauti kama jibu na radiamali ya kundi hilo kwa matamshi ya Abu Mus'ab al Barnawi ambaye amejitangaza kuwa kiongozi mpya wa kund hilo magharibi mwa Afrika na kueleza kuwa, wanachama wa Boko Haram hawamkubali mtu yoyote kuwa kiongozi wao mpya.

 

Abu Mus'ab al Barnawi ambaye inasemekana amejiarifisha kuwa kiongozi mpya wa Boko Haram

Shekau ambaye analiongoza kundi la Boko Haram tangu mwaka 2009 ametangaza kuwa watu wanapaswa kuelewa kuwa kundi la Boko Haram bado lipo na kwamba limepinga uamuzi huo wa Daesh wa kumuengua uongozini. Itakumbukwa kuwa mwezi Machi mwaka jana kundi la Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh. Aidha hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa Abubakar Shekau ameuawa huku jeshi la Nigeria likitangaza mara kadhaa kumuua kinara huyo wa Boko Haram.

Abu Mus'ab al Barnawi alikuwa msemaji wa kundi la Boko Haram.