Sep 06, 2016 07:46 UTC
  • Mapigano kati ya waasi na vikosi vya jeshi huko Walikale Kongo DR

Watu wawili wameuawa kwenye mapigano kati ya waasi na vikosi vya jeshi la Kongo katika eneo la Walikale nchini humo.

 

Duru za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimearifu kuwa raia wawili waliuawa jana katika mapigano kati ya askari jeshi wa Kongo na waasi wa Mai-Mai Mazembe katika wilaya kadhaa za eneo la Walikale mkoani Kivu ya Kaskazini nchini Kongo. Duru hizo zimeongeza kuwa mapigano hayo yamejiri kufuatia shambulio lililofanywa na waasi wa Mai-Mai Mazembe juzi Jumapili katika kambi za jeshi la Kongo katika eneo la Kateku karibu na maeneo ya Walikale na Lubero.

Waasi wa Mai-Mai Mazembe

Watu walioshuhudia mapigano hayo wamesema kuwa, kambi ya jeshi la Kongo imechomwa moto na waasi wa Mai-Mai Mazembe na baadhi ya wakazi kulazimika kuvihama vijiji vyao na kukimbilia porini. Duru za kijeshi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesisitiza kuwa wanajeshi wengi wametumwa huko Walikale ili kuongeza nguvu katika kikosi kinachopambana na waasi hao.

Tags