Sep 18, 2016 07:16 UTC
  • Vijiji vinne vyakombolewa kaskazini mashariki mwa Kongo DR

Duru za kijeshi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimearifu kukombolewa vijiji vinne kaskazini mashariki mwa nchi hiyo vilivyokuwa vimetekwa na waasi.

Duru hizo zimeeleza kuwa wanajeshi wa Kongo wamefanikiwa kuvikomboa vijiji vinne katika eneo la Mambasa mkoani Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Vijiji hivyo vinne vilikuwa vinashikiliwa na waasi wa Mai-Mai kwa miezi kadhaa.

Waasi wa Mai-Mai ambao wamekuwa wakivuruga hali ya usalama  mashariki mwa Kongo 

Duru za kijeshi za Kongo zimeongeza kuwa kikosi cha 31 cha jeshi la nchi hiyo kimekuwa kikiendesha oparesheni dhidi ya ngome za waasi wa Mai-Mai katika eneo la Mambasa tangu wiki mbili zilizopita. Afisa mmoja wa jeshi la Kongo katika eneo la Mambasa ameeleza kuwa waasi 67 wa Mai-Mai wametiwa nguvuni katika oparesheni hiyo ya jeshi na bunduki 16 na silaha nyingine zimenaswa pia kupitia oparesheni hiyo.

Tags