Touadera apata ushindi wa mapema katika uchaguzi wa rais CAR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1567-touadera_apata_ushindi_wa_mapema_katika_uchaguzi_wa_rais_car
Faustin Archange Touadera, Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amepata ushindi wa mapema katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili iliyopita ya Februari 14.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 19, 2016 23:37 UTC
  • Touadera apata ushindi wa mapema katika uchaguzi wa rais CAR

Faustin Archange Touadera, Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amepata ushindi wa mapema katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili iliyopita ya Februari 14.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa, Touadera amepata zaidi ya kura laki moja na 20 elfu katika matokoe ya awali ya kura zilizopigwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, dhidi ya hasimu wake Anicet Georges Dologuele ambaye amepata kura 55,000. Duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati inaonekana kuwa ni hatua muhimu ya kurejesha utawala wa kidemokrasia na kumaliza miaka kadhaa ya vita vilivyoleta mpasuko na migawanyiko nchini humo. Wagombea wote wawili ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu huko nyuma, walilipa kipaumbele suala la kurejesha amani na usalama katika kampeni zao. Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ni moja ya nchi zisizo na uthabiti zaidi duniani, mnamo mwaka 2013 ilitumbukia kwenye mgogoro mbaya zaidi katika historia yake baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Francois Bozize kuondolewa madarakani.