Jan 04, 2017 16:22 UTC
  • Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
    Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameendelea kupambana na waasi wa Mai Mai, mashariki mwa nchi hiyo.

Vyombo vya habari veneo hilo vimeripoti habari hiyo na kusema kuwa, wanajeshi wa serikali wamepambana na waasi wa Mai Mai katika mkoa wa Kivu Kusini ambapo mwanajeshi mmoja wa serikali ameuawa.

Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya kieneo, wanajeshi wawili wa serikali hawajulikani walipo kutokana na mapigano hayo ya siku mbili yaliyotokea kwenye kijiji cha Yungu kwenye eneo la Fizi la mkoa wa Kivu Kusini.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

 

Mapigano hayo yamezusha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mashuhuda walionukuliwa na vyombo hivyo vya habari wamesema kuwa, waasi wa Mai Mai walikiteka kijiji cha Yungu kwa masaa kadhaa, lakini wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuwafurusha waasi hao na kukikomboa kijiji hicho.

Waasi wa Mai Mai

 

Hii ni katika hali ambayo askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wametumwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu mwaka 1999 lakini hadi hivi sasa wameshindwa kuirejesha kwenye amani nchi hiyo kubwa ya katikati mwa Afrika. 

Jukumu la maafisa wa kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa ambao wanakadiriwa kufikia wanajeshi 20 limetajwa kuwa ni kuwapokonya silaha waasi, lakini hadi leo hii wameshindwa kufanikisha jukumu hilo.

 

Tags