Jeshi la Somalia lakomboa eneo la mpakani kutoka kwa al Shabab
Jeshi al Somalia limefanikiwa kukomboa eneo la mpaka wa nchi hiyo na Kenya lililokuwa limetekwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab.
Maafisa wa serikali ya Somalia wametangaza kuwa, eneo la Bulla Hawa lilikombolewa jana siku moja tu baada ya kuvamiwa na kutekwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab.
Kundi la al Shabab Jumatatu iliyopita liliua askari 24 wa Somalia kwa kulipua gari lililokuwa limetegwa mabomu katika eneo la Bulla Hawa na baadaye liliwarejesha nyuma askari wa mpakani wa Kenya baada ya kuteka kambi ya jeshi la Somalia katika eneo hilo.
Mashambulizi ya kigaidi la kundi la al Shabab yanayoendelea kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi sasa nchin Somalia yameua maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni ya Wasomali kuwa wakimbizi.