New York Times: Maelfu ya watu wamenasa katika utumwa Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36539-new_york_times_maelfu_ya_watu_wamenasa_katika_utumwa_uingereza
Ripoti iliyochapishwa na tume ya serikali ya Uingereza imesema kuwa maelfu ya watu nchini humo wanatumbukia katika mtego wa utumwa na kwamba baadhi yao ni wahajiri japokuwa wengi wao ni raia wa Uingereza yenyewe, suala ambalo limezusha mshtuko mkubwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 19, 2017 23:18 UTC
  • New York Times: Maelfu ya watu wamenasa katika utumwa Uingereza

Ripoti iliyochapishwa na tume ya serikali ya Uingereza imesema kuwa maelfu ya watu nchini humo wanatumbukia katika mtego wa utumwa na kwamba baadhi yao ni wahajiri japokuwa wengi wao ni raia wa Uingereza yenyewe, suala ambalo limezusha mshtuko mkubwa.

Ripoti hiyo iliyochapishwa na gazeti la New York Times la Marekani imesema kuwa, aghlabu ya wahanga wa biashara ya utumwa nchini Uingereza ni Waingereza ambao wanatumiwa katika masuala mbalimbali.

Ripoti hiyo imesema kuwa, baadhi ya wahanga hao wanatumiwa katika saluni na kumbi za kusafisha kucha na miguu, kuosha magari na mashambani. Imeongeza kuwa maelfu ya watoto wanauzwa kama bidhaa na mara nyingi hukabiliana na unyama na ukatili.

Utumwa mamboleo nchini Uingereza

Ripoti hiyo ya tume ya serikali ya Uingereza imesisitiza kuwa maelfu ya watu wenye umri tofauti wanatumbukia katika utumwa nchini humo kwa njia moja au nyingine na kutokana na sababu tofauti za kiutamaduni, umaskini, kufeli katika masomo, dawa za kulevya na kadhalika.