Malawi yatangaza maafa katika wilaya 20 za nchi hiyo
Malawi ambayo tayari inayosumbuliwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi, imetangaza maafa katika wilaya 20 baada ya uharibifu mkubwa wa mazao ya kilimo uliosababishwa na hujuma ya wadudu wanaoharibu mazao na kutishia usalama wa chakula.
Wadudu hao ambao wamevamia nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini wameshambulia wilaya 20 kati ya wilaya zote 28 za Malawi na kuathiri maelfu ya hektari za mashamba ya kilimo, suala ambalo linatishia usalama wa chakula nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Malawi imesema kuwa: "Nchi inakabiliwa na uharibu mkubwa wa mazao ya kilimo unaotishia ualama wa chakula ambao utaathiri raia wengi."

Malawi ambayo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi dunianin inakabiliwa na upunguvu mkubwa wa chakula kutokana na uhaba wa mvua. Nchi hiyo pia imekumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya vya watu kadhaa na kuzilamisha familia zaidi ya 200 kuhama makazi yao.