Uganda yatuma askari Tanzania katika mazoezi ya kijeshi ya Afrika Mashariki
(last modified Fri, 02 Nov 2018 06:04:53 GMT )
Nov 02, 2018 06:04 UTC
  • Uganda yatuma askari Tanzania katika mazoezi ya kijeshi ya Afrika Mashariki

Uganda imetuma askari na raia 219 kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Tanzania.

Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Kanali Deo Akiiki amesema mazoezi hayo yanayoshirikisha askari na raia elfu moja kutoka Uganda, Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini na Tanzania ni pamoja na operesheni za kuunga mkono amani, usimamizi wa maafa, vita dhidi ya ugaidi na uharamia.

Mazoezi hayo yalianza kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kwa lengo la kuimarisha uwezo wa majeshi ya nchi wanachama katika kulinda amani ili kuzuia matukio chungu katika eneo hilo kama tukio la mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.

 

Tags