Ennahdha: Kunafanyika njama za kutaka kumuua Rais Essebsi wa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54503-ennahdha_kunafanyika_njama_za_kutaka_kumuua_rais_essebsi_wa_tunisia
Mwenyekiti wa chama cha Kiislamu cha al Ennahdha nchini Tunisia amesema kuwa kunafanyika jitihada za kumuua Rais Beji Caid Essebsi wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 02, 2019 03:49 UTC
  • Ennahdha: Kunafanyika njama za kutaka kumuua Rais Essebsi wa Tunisia

Mwenyekiti wa chama cha Kiislamu cha al Ennahdha nchini Tunisia amesema kuwa kunafanyika jitihada za kumuua Rais Beji Caid Essebsi wa nchi hiyo.

Rached Ghannouchi amesema kuwa, hakuna taarifa kamili kuhusiana na hatua iliyofanywa na baadhi ya watu ya kumpa sumu Rais Beji Caid Essebsi lakini si mbali kwamba kunafanyika njama za kutaka kumfutilia mbali.

Al Ghanuushi amesema baadhi ya watu wanaamini kuwa, Beji Caid Essebsi ni nguzo ya mfumo wa kidemokrasia wa Tunisia, hivyo si jambo lililombali kwamba wapinzani wa demokrasia wanataka kumfutilia mbali.

Mwenyekiti wa chama cha Ennahdha amesema kuwa, madai yaliyotolewa na baadhi ya wataalamu wa sheria kuhusu kuwepo ombwe la kisheria nchini Tunisia kutokana na hali mbaya ya kiafya ya Rais Beji Caid Essebsi ni sehemu ya njama hizo zilizodhidi ya demokrasia.

Beji Caid Essebsi

Amesisitiza kuwa hakuna ombwe la kisheria nchini Tunisia na iwapo itathibitika kuwa Rais wa nchi hana uuwezo wa kutekeleza majukumu yake Bunge litachukua madaraka ya nchi.

Siku chache zilizopita Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia alilazwa katika hospitali moja mjini Tunis kutokana na hali yake mbaya ya kiafya. Essebsi mwenye umri wa miaka 93 anaiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2014.