Jul 15, 2019 11:32 UTC
  • Mark Lowcock
    Mark Lowcock

Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huwenda ukaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu, kuua idadi zaidi ya watu na kugharibu fedha nyingi iwapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa hazitatoa mamia ya mamilioni ya dola kwa sasa kwa ajili ya kupambana na kasi ya ugonjwa huo.

Mark Lowcock ambaye alikuwa akizungumza na vyombo vya habari kabla ya mkutano wa Geneva ulioitishwa kwa ajili ya kukusanya fedha za kukabiliana na mlipuko wa Ebola huko Congo DR, amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia jitihada za kukomesha ugonjwa huo.

Mapema mwezi uliopita Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema karibu robo ya watu walioambukizwa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamkini hawajui kwamba wanaugua ugonjwa huo hatari.

Katika taarifa yake WHO ilisema kuwa mtu mmoja kati ya kila watu wanne mashariki mwa DRC, ameambukizwa ugonjwa hatari wa Ebola lakini hafahamu.

Ugonjwa wa Ebola unaendeelea kuua watu Congo DR

WHO imesema hilo wakati huu inapoendelea kusaidia kupambana na maambukizi ya Ebola hasa mjini Beni, ambapo watu zaidi ya 2,000 wameambukizwa na wengine 1,357 wamepoteza maisha tangu mwezi Agosti mwaka 2018.

Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC pia imetahadahrisha kuhusu tishio la ugonjwa hatari wa Ebola kuenea katika nchi za jumuiya hiyo hususan baada ya kugundulika kesi kadhaa za watu waliopatwa na Ebola nchini Uganda.   

Tags