Marekani, EU: Tunawaunga mkono mabaradhuli wa Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56574-marekani_eu_tunawaunga_mkono_mabaradhuli_wa_uganda
Marekani na nchi za Ulaya zimetiwa kiwewe na azma ya Uganda ya kutoa adhabu ya kifo kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki vitendo vya ubaradhuli nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 12, 2019 04:35 UTC
  • Marekani, EU: Tunawaunga mkono mabaradhuli wa Uganda

Marekani na nchi za Ulaya zimetiwa kiwewe na azma ya Uganda ya kutoa adhabu ya kifo kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki vitendo vya ubaradhuli nchini humo.

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema, "Tunatathmini kwa karibu matukio yanayojiri nchini Uganda. Marekani inapinga kufanywa uhalifu vitendo vya watu wa jinsia moja kuwa na uhusiano. Tunasimama na jamii ya LGBT nchini Uganda na tunatumai haki zao zitaheshimiwa."

Kadhalika Umoja wa Ulaya umetishia kuikatia nchi hiyo ya Afrika Mashariki misaada ya mamilioni ya dola iwapo itapasisha na kuanza kutekeleza sheria hiyo.

Misimamo hiyo ya Marekani na Ulaya ya kuunga mkono mabaradhuli wa Uganda imekuja baada ya serikali ya Kampala kutangaza nia yake ya kurejesha muswada bungeni ambao utatoa adhabu kali kwa mabaradhuli na wanaoendesha vitendo vichafu vya mahusiano ya watu wa jinsia moja.

Bunge la Uganda

Muswada huo ambao huko Uganda unajulikana kwa jina maarufu la “Ua Mabaradhuli” ulikataliwa bungeni miaka mitano iliyopita kutokana na matatizo ya kiufundi. Hata hivyo siku ya Alkhamisi serikali ya Uganda ilisema kuwa ina mpango wa kuurejesha bungeni muswada huo katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Serikali ya Uganda inasema vitendo hivyo vichafu vimeenea sana nchini humo na inabidi sheria kali ziwekwe kudhibiti ngono hizo zilizo kinyume na maumbile.