Watu wenye silaha washambulia magharibi mwa Madagascar, waua na kujeruhi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i5899-watu_wenye_silaha_washambulia_magharibi_mwa_madagascar_waua_na_kujeruhi
Watu wenye silaha wamefanya shambulizi magharibi mwa Madagascar na kuua watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 27, 2016 02:55 UTC
  • Watu wenye silaha washambulia magharibi mwa Madagascar, waua na kujeruhi

Watu wenye silaha wamefanya shambulizi magharibi mwa Madagascar na kuua watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa katika eneo hilo.

Polisi ya nchi hiyo imeripoti kuwa, watu wenye silaha wamemshambulia mkuu wa ofisi ya ardhi katika eneo la Melaky na kumuua pamoja na rafiki yake. Katika hujuma hiyo watu wengine kadhaa pia wamejeruhiwa. Polisi wamesema kuwa, washambuliaji hao walianza kufyatua risasi kuilenga gari iliyokuwa imembeba afisa huyo wa ardhi pamoja na watu wengine aliokuwa ameambatana nao. Habari zaidi zinasema kuwa, licha ya polisi kufika eneo la tukio mapema, lakini walishindwa kukabiliana na watu hao wenye silaha, huku wakitoweka bila ya kutiwa mbaroni. Polisi imetangaza kuwa inaendelea kuwasaka wahusika wa hujuma hiyo, ambayo hadi sasa bado sababu za utekelezwaji wake hazijulikani, ingawa masuala ya kisiasa yanatajwa kuwa moja ya sababu hizo.