Ufaransa na nchi nyingine 12 zakubaliana kuanzisha Takuba kukabiliana na ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60040-ufaransa_na_nchi_nyingine_12_zakubaliana_kuanzisha_takuba_kukabiliana_na_ugaidi
Ufaransa na nchi nyingine 12 zimekubaliana kuanzisha kikosi kipya kitakachopewa jina la Takuba kwa shabaha ya kukabiliana na makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel barani Afika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 29, 2020 05:09 UTC
  • Ufaransa na nchi nyingine 12 zakubaliana kuanzisha Takuba kukabiliana na ugaidi

Ufaransa na nchi nyingine 12 zimekubaliana kuanzisha kikosi kipya kitakachopewa jina la Takuba kwa shabaha ya kukabiliana na makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel barani Afika.

Mawaziri wa ulinzi na wawakilishi wa nchi 13 wametoa taarifa ya kisiasa wakisisitiza kuwa nchi zao zitaendeleza juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel Afrika.

Nchi hizo 13 zinajumuisha Ufaransa, Jamhuri ya Czech, Denmark, Estonia, Ubelgiji, Ujerumani, Mali, Uholanzi, Niger, Norway, Ureno, Sweden, Chad na Uingereza.

Ufaransa ina karibu askari 4,500 katika eneo la Sahel Afrika, na kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Florence Parly, wanajeshi wengine 600 watatumwa katika eneo hilo kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi.

Ufaransa imekuwa ikizihimiza nchi za Ulaya kusaidia operesheni ya kijeshi katika eneo hilo la katikati na kaskazini mwa Afrika ikisisitiza kuwa, kuwepo magaidi katika eneo hilo la Afrika kunahatarisha usalama wa nchi za Ulaya.

Askari wa nchi za Magharibi katika eneo la Sahel Afrika

Wachambuzi wa mambo wanasisitiza kuwa, juhudi hizo za Ufaransa zinafanyika kwa ajili ya kulinda miradi ya makampuni ya Ufaransa na nchi nyingine za Maghaibi yanayochimba madini na mafuta katika nchi za Afrika. Baadhi ya nchi za Afrika pia zinaikosoa Ufaransa kutokoana na kuingilia masuala ya ndani ya nhi hizo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.