Rais Kais Saied wa Tunisia: Kuna mpango wa kutaka kuniua
-
Rais Kais Saied
Rais Kais Saied wa Tunisia ameyatuhumu makundi ya kisiasa kwamba yanapanga mikakati ya kutoa dhoruba dhidi ya serikali yake ikiwa ni pamoja na mpango wa kutaka kumuua yeye mwenyewe.
Kais Saied ametishia kwamba anayo makombora ya kutosha ambayo yako tayari kwa ajili ya kushambulia ngome za maadui wake.
Amewatuhumu baadhi ya wanasiasa kwamba wanazichochea nchi za kigeni dhidi yake na nchi ya Tunisia na kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Nchi ya Tunisia imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa baada ya Rais Kais Saied wa nchi hiyo kumfuta kazi waziri mkuu, kusimamisha shughuli za Bunge la kutwaa madaraka yote ya nchi.
Spika wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi amesema hatua aliyochukua Rais Kais Saied ni mapinduzi dhidi ya mapinduzi ya wananchi, katiba ya nchi na uhuru wa taifa.
Vilevile Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki amekosoa sera na maamuzi ya Rais Kais Saied na kusema hatua hizo ni sawa na mapinduzi na udikteta na kwamba ni ufisadi mbaya zaidi.