Jun 01, 2016 15:28 UTC
  • Kumalizika maambukizo ya Ebola nchini Guinea Conakry

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza habari ya kumalizika maambukizo ya homa hatari ya Ebola huko Guinea Conakry.

Aidha shirika hilo limetahadharisha kuhusu hatari ya kurejea ugonjwa wa Ebola na kueleza kuwa, mambukizo ya mwisho ya homa ya Ebola huko Guinea Conakry yaliripotiwa mwezi Aprili, na ni siku 42 sasa zimepita, nchi hiyo haina kesi yoyote ya maradhi hayo.

Bekr Gaye, Mjumbe wa Guinea Conakry katika Umoja wa Mataifa amewataka raia wa nchi hiyo kujiepusha na jambo lolote linalotishia kurejea homa ya Ebola nchini humo. Kesi mpya za maambukizo ya Ebola ziliripotiwa baada ya kutangazwa kutokomezwa homa hatari ya Ebola huko Liberia, Sierra Leone na Guinea Conakry nchi tatu zilizoathiriwa vibaya na Ebola huko magharibi mwa Afrika. Homa hatari ya Ebola ilianza kwa mara ya kwanza huko Guinea Conakry mwaka 2013 na tangu wakati huo hadi hivi sasa, watu zaidi ya elfu 11 wameaga dunia kwa maradhi hayo.

Tags