Mgogoro wa Libya; na kuanza mazungumzo ya nchi hiyo mjini Geneva
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i85280-mgogoro_wa_libya_na_kuanza_mazungumzo_ya_nchi_hiyo_mjini_geneva
Umoja wa Mataifa umewataka viongozi wa Libya kuonyesha jitihada zao za dhati na kijasiri katika mazungumzo ya makundi ya kisiasa ya nchi hiyo mjini Geneva Uswisi kwa ajili ya kuinasua nch hiyo katika mkwamo wa uchaguzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 28, 2022 23:03 UTC
  • Mgogoro wa Libya; na kuanza mazungumzo ya nchi hiyo mjini Geneva

Umoja wa Mataifa umewataka viongozi wa Libya kuonyesha jitihada zao za dhati na kijasiri katika mazungumzo ya makundi ya kisiasa ya nchi hiyo mjini Geneva Uswisi kwa ajili ya kuinasua nch hiyo katika mkwamo wa uchaguzi.

Stephanie Williams Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Libya alisema jana wakati wa kuanza mazungumzo hayo huko Geneva kwamba: viongozi wa Libya sasa wamefikia katika marhala nyeti baada ya kuvuka nje ndefu na ngumu; na kwamba umefika wakati sasa wa kufikiwa mapatano ya kihistoria  kwa maslahi ya Libya, wananchi na taasisi za nchi hiyo.  

Aguilah Saleh Spika wa Bunge la Libya na Khalid al Mishri Mkuu wa Baraza Kuu la Uongozi la nchi hiyo watakuwa na mazungumzo katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuhusu rasimu ya fremu ya katiba kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wa Libya.  

Aguilah Saleh, Spika wa Bunge la Libya 

Awali uchaguzi wa rais na bunge wa Libya ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka jana ili kukamilisha kikamilifu mchakato wa amani uliokuwa ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa baada machafuko ya mwaka 2020. 

Hata hivyo uchaguzi huo umeakhirishwa kwa muda usiojulikana kutokaa na kushadidi hitilafu kati ya mirengo ya kisiasa na mapigano ya mara kwa mara ya makundi hasimu ya wanamgambo wenye silaha huko Tripoli mji mkuu wa Libya.